FALSAFA

FALSAFA ZA SENSEI SHIGERU EGAMI KUHUSIANA NA MAFUNZO YA SANAA ZA MAPIGANO

Huko China, magombo mwawili marufu kuhusu sanaa za mapigano ni Ekkin Gyo na Ekkin Zenkui. Wanazuoni wengi wanaamini kwamba Daruma(Bodhi Dharma) ndiye aliye viandika vitabu hivyo katika hekalu la Shaolin. Magombo haya yanaeleza ni kwa namna gani mtu anatakiwa kujifunza huku akiitakasa nafsi yake. Inaaminiwa kwamba Karate-do ilizaliwa kutoka kwenye mtazamo huu.

(Inasadikika Bodhi Dharma ndiye aliye ipeleka sanaa ya mapigano huko China kutokea India katika harakati za kuhubiri dini ya Budha kwenye mahekalu ya Shaolin takriban miaka 1,500 iliyopita)

Kwa mafunzo na mazoezi, matatizo hupata suluhu.
Adui wa kwanza ni nafsi yako!
Lengo kuu la Karate-Do ni kupigania mwenendo sahihi wa tabia(kupigania tabia njema).
Ukijaribu kuyapunguza madhaifu yako katika kila siku ya maisha yako.
Ni nini maana ya upatanisho? Ni nini maana ya maisha? Amani ni nini? Umoja ni nini?
Natamani kuelewa uhusiano baina ya watu, baina ya watu na uasili wa mazingira yao.
Mwili na roho ni kitu kimoja.
Uimarishwaji wa mwili hukuza akili. Mwili uliozorota huzorotesha akili. Hiyo ndiyo sababu kuu iliyo
msukuma Daruma(Bodhi Dharma) kuanzisha mafunzo ya sanaa za mapigano katika hekalu la Shaolin takriban miaka 1500 iliyopita.
Ni kwa mazoezi ndipo utapomudu ustadi wa mbinu. Lakini kamwe lengo la jitihada zako halitakiwi liwe ni kujionyesha au Kupoteza amani. Kutokana na uasili wa binadamu, ni vigumu mno akaishi peke yake. Binadamu anahitaji utulivu wa nafsi lakini wakati huohuo anawajibika kuwapa amani wale wanaomzunguka. Atatakiwa awatendee wengine kama ambavyo yeye angependa kutendewa.
Unajaribu kuwaelewa wengine kwa kuielewa nafsi yako kwanza. Hii ndio njia ya mafunzo. Natumaini wote tutajifunza huku tukizikagua nafsi zetu katika kupigania mwenendo sahihi wa tabia.

MIONGOZO 22 YA MEIJIN GICHIN FUNAKOSHI

1. Karate huanza na kumalizika kwa nidhamu.
2. Daima fikiri kiubunifu.
3. Fikra huja kabla ya mwili.
4. Jiweke tayari kuwa huru kifikra.
5. Jitambue kwanza ndio uwatambue wengine.
6. Karate ni muongozo wa haki na inapaswa kutumika hivyo tu.
7. Sogea kufuatana na mpinzani wako.
8. Kamae ni kwa wanafunzi wapya na shizentai ni kwa wazoefu.
9. Usifikirie kwamba inabidi ushinde ila fikiri kwamba hupaswi kushindwa.
10. Karate si katika Dojo peke yake.
11. Husisha karate katika kila jambo ulifanyalo, wakati wote fikiri kuitumia miongozo hii kila siku.
12. Mafunzo ya karate ni ya wakati wote wa maisha yako.
13. Karate ni kama maji ya moto, yasipoendelea kupashwa moto au kuhifadhiwa na joto lake, hupoa.
14. Mara tu utokapo nyumbani, una wapinzani zaidi ya elfu moja.
15. Hakuna shambulio la kwanza kwenye karate.
16. Elewa tofauti ya sehemu zenye madhara na zisizo na madhara.
17. Uzembe huja kabla ya ajali.
18. Fikiri mikono na miguu yako kuwa kama sime.
19. Kumbuka vipengele vigumu na vyepesi kwenye kata.
20. Karate ikifanyika vyema ni tofauti na kombati(struggle fighting).
21. Jihadhari na matendo yako, usije ingia matatani.
22. Mafunzo ya kata si uhalisi wa jambo lenyewe.

1 comment: