Saturday, June 5, 2010

MATUMIZI YA 'HIP' KATIKA MAKIWARA

HATUA YA KWANZA


HATUA YA PILI


HATUA YA MWISHO

KAZI YA MGUU UNAOBAKI NYUMA..

Mguu unaobaki nyuma unakazi ya kusinyaa(kukunjika) wakati wa kukinga shambulizi, na kufyatuka

mithili ya spring, wakati wa kushambulia au kutoa shambulizi.

Kwa namna hiyo, unakisaidia kiuno katika mzunguko wake kutoka hanmi kwenda shomen. Na hii

huongeza nguvu mno katika shambulizi na kusaidia shambulizi kufika katika shabaha iliyokusudiwa.

Ustadi huu ni wa kukumbukwa kila siku katika mafunzo ya sanaa hii ya mapigano.

ANGALIA KWA MAKINI MABADILIKO YA MSTARI MWEKUNDU








MFANO MWEPESI WA MATUMIZI YA 'HIP'

Hapa tunaona katika sotouke, Sensei Yahara yuko hanmi(kiuno chake kaelekea nyuzi 45 kutoka kwa

mpinzani wake-Norio Kawasaki san).

Alkadhalika, katika gyakuzuki, Sensei Yahara yuko shomen(kiuno chake kinaelekea mbele, kwa

mpinzani wake-Sensei Kawasaki).

Karibu mbinu zote zinazo husisha kukinga na kushambulia zinatakiwa zifuate mtiririko huu, yaani

gedanbarai-gyakuzuki, chudan uchiuke-gyakuzuki, ageuke-gyakuzuki nakadhalika.

'HANMI'


'SHOMEN'

HIP!.....HIP!....HIP!!!

Kimsingi, mbinu yoyote ya Karate inatakiwa ihusishe 'hip' au kiuno kwa Kiswahili chepesi.

Walimu wa kale wa Karate walizoea kusema "kinga kwa kutumia 'hip', piga ngumi kwa kutumia 'hip',

piga teke kwa kutumia 'hip'.....".


'Hip' inatoa mchango mkubwa sana wa nishati katika shambulizi kama ikitumiwa vizuri.

Alkadhalika, matumizi ya 'hip' husaidia shambulizi kufika kwenye shabaha iliyo kusudiwa.

Kunawakati karateka hushambulia lakini kwasababu hakutumia 'hip', shambulizi lake huweza

kuishia hewani na hivyo kupoteza nishati pasipo sababu.

Lakini kamwe ustadi wake si wa kuumudu kwa siku mbili au miezi. Ni ustadi ambao karateka

anapaswa kuutafuta kwa miaka ili ifike wakati ambapo ataweza kuuonyesha hata pasipo tahadhari.

Inakuwa ni kawaida yake kutumia 'hip' katika kila mbinu ya Karate anayoitumia.

Hiyo pia huonyesha ni kwa-kiasi gani karateka huyo alivyo 'balehe' kwenye sanaa ya mapigano.

HATUA YA KWANZA YA MZUNGUKO WA 'HIP'

HATUA YA PILI YA MZUNGUKO WA 'HIP'


MWISHO WA SHAMBULIZI

MJUE SENSEI MIKIO YAHARA

SENSEI YAHARA AKIWA KWENYE 'UNSU'

SENSEI MIKIO YAHARA KATIKA 'MAKIWARA'

Mikio Yahara ni moja ya walimu hodari na waliojizolea umaarufu katika ulimwengu wa Karate.

Makarateka wengi waliokutana nae katika programu za Karate, huelezea ni kwa kiasi gani anaweza

kutumia mbinu ambazo ni ngumu kufikirika lakini pia ni kwa namna gani anaweza kuwa 'mkatili' na

mwenye 'kuogopesha' katika makabiliano.



Mikio Yahara alizaliwa mwaka 1947, huko Ehime, Japani. Alimaliza masomo yake ya elimu ya juu

katika chuo kikuu cha Kokushinkan, ambako pia alijiunga na kozi maarufu ya ualimu ya JKA.


Mikio pia anaheshimika kwa uwezo aliouonyesha katika 'Unsu', jinsi anavyo tumia nishati, wepesi

na morali kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa kata.


Mwaka 2000, Yahara alianzisha shirikisho lake liitwalo Karatenomichi World Federation baada

ya kutoka kwenye migogoro ya JKA.

Falsafa ya shirikisho lake ni 'shambulizi la kuua' au 'hikken hisatsu'.

Imelenga katika kuimarisha mashambulizi ya karateka na hatimaye kufikia uwezo wa kuua kwa shambulizi

moja tu.


Pamoja na tofauti zetu, lakini hatuwezi kukataa uhodari aliouonyesha Sensei Mikio Yahara katika

sanaa hii ya mapigano.