SENSEI NI NANI ?
Huko Japani kila mwalimu huitwa Sensei. Lakini pia mwanasheria au daktari huitwa Sensei kutokana na
kwamba ni msomi au mjuzi wa maarifa kuliko walio wengi.Pia  kama ilivyo ada kwamba wanasheria wengi hujihusisha na maswala ya siasa hivyo huko Japani kunawakati mwanasiasa  pia huitwa Sensei .
Lakini labda wengi wamewahi kujiuliza kwamba ni sifa zipi hasa zinazomfanya mtu awe Sensei?
Watu wanaoitwa Sensei wanatakiwa kuishi kama walimu katika maisha yao yote. 
Kimsingi neno Sensei limetokana na maneno mawili ya kijapani  yaani ‘sen’ na ‘sei’.
i) ’sen’ maana yake ni kabla.
ii)’sei’ maana yake ni kuzaliwa.
Hivyo Sensei ni mtu ambaye amezaliwa kabla(kifikra) au mtu aliyepata ujuzi wa jambo fulani kabla ya
 wengine. Heshima ni moja ya vigezo vikubwa sana kwa mtu anayeitwa Sensei. 
Anatakiwa kuheshimu kila kiumbe chenye uhai. Hii ni kwa sababu heshima ni kitu muhimu sana 
katika kujenga uhusiano mzuri miongoni mwa viumbe hai akiwemo binadamu.  
Mara nyingi kwenye karate cheo cha usensei hutolewa katika mazingira yafuatayo :-
1)Karateka aliye kwenye  daraja la mkanda mweusi na ana wanafunzi ambao yeye kama mwalimu
    huwafundisha na kuyaishi yale anayoyafundisha. Huyu anapaswa kuitwa Sensei haswa na wanafunzi
    wake.  Si lazima kuitwa Sensei na kila karateka ila wanafunzi wake.
2)Karateka aliye kwenye  daraja la mkanda mweusi na aliyeteuliwa na shirikisho fulani la kitaifa
   au kimataifa kuwa Sensei. Huyu kwa heshima na taadhima anapaswa kutambuliwa kama
  Sensei na karateka yeyote.
No comments:
Post a Comment