BAADHI YA SABABU ZA STAILI NYINGI ZA KARATE KUCHEZWA PEKU(PASIPO VIATU)
i)Utamaduni wa wajapani.
   Wajapani huvua viatu kabla ya kuingia kwenye nyumba zao. Hivyo basi kutokana na kwamba
    karate imechukua sehemu kubwa sana ya utamaduni wa wajapani, kuvua viatu kabla ya
    mafunzo ni itifaki mojawapo inayopaswa kuzingatiwa. Baadhi ya itifaki nyingine ni kusalimia
    au kutoa heshima kwa kuinamisha kichwa, kutamka mbinu za karate kwa lugha ya kijapani n.k.
ii)Kuimarisha miguu.
    Hii ni pamoja na kuongeza usugu na unene wa ngozi ya mguu.
iii)Kupunguza eneo la sehemu ya mguu inayoshambulia.
    Kwenye fizikia  imedhihirishwa  kwamba mgandamizo huongezeka kutokana na kupungua kwa
    eneo. Hivyo basi ili kuongeza madhara ya shambulizi katika shabaha au eneo  lililokusudiwa, ni
    vyema eneo la kushambulia likapunguzwa kadri iwezekanavyo.
iv)Msafirisho wa nishati(ki) kutoka ardhini.
    Mgusano baina ya unyayo na ardhi hurahisisha usafirishaji wa nishati isiyoelezeka kwa urahisi kutoka
    ardhini na kuingia kwenye mwili. Ukufunzi wangu hautoshi katika kulielezea jambo hili.
KIHON NI NINI?
Kihon ni neno la kijapani linalo maanisha mbinu za msingi. Hii ni pamoja na upigaji wa ngumi au teke,
namna ya kupangua ngumi au teke, matumizi ya sehemu mbalimbali za mwili katika ushambuliaji.
SENPAI  au SEMPAI NI NANI ?
Senpai ni neno la kijapani lenye maana ya mtu anaye simamia mafunzo ya karate kwa niaba ya Sensei.
‘Sen’ maana yake ni ‘kabla’ kama ilivyo kwa Sensei na ‘pai’ maana yake ni ‘kundi’. Hivyo senpai ni mtu
 anayesimamia kundi fulani kutokana na kwamba ni mjuzi wa maarifa kuliko walio wengi katika kundi.
No comments:
Post a Comment