Pages

Thursday, March 17, 2011

SHIHAN MANABU MURAKAMI

Sensei Manabu Murakami anashikilia daraja la saba la mkanda mweusi
( dani saba) kutoka shirikisho la SKIF lililo anzishwa na Kancho
Kanazawa Hirokazu(dani kumi). Sensei Manabu amewahi kutwaa taji
la kombe la dunia la Karate(SKIF) mara mbili ikiwa ni pamoja na
rekodi zifuatazo:-

Mashindano ya tatu ya SKIF, Timu ya Kata na Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya nne ya SKIF, Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya tano ya SKIF, Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya saba ya SKIF, Timu ya Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya nane ya SKIF, Kumite...Mshindi wa kwanza.

Murakami Sensei alizaliwa mwezi wa kumi, mnamo mwaka 1966 Kyushu,
kusini mwa Japan. Alianza kujihusisha na Karate akiwa na umri wa
miaka tisa chini yausimamizi wa Sensei Maruo aliyekuwa mwalimu
wa JKA. Kacho Kanazawa alipo unda shirikisho la SKIF mnamo mwaka
1978, bila kusita Sensei Manabu Murakami akajiunga na SKIF na
kujitoa JKA. Baada ya kumaliza masomo yake katika chuo kikuu cha
Takushoku,Sensei Murakami akaamua kujiunga na kozi ya ualimu ya
SKIF ambayo aliihitimu baada ya miaka miwili. Baada ya hapo Sensei
Murakami akaamua kufundisha katikadojo kuu ya SKIF (Japan) ambako
yuko mpaka leo hii.

Sensei Manabu Murakami anashauri wanafunzi wafurahie mafunzo ya
Karate,iwe ni moja ya burudani sambamba na kuwa taaluma. Kwa namna
hiyo ana amini mwanafunzi ataweza kufika mbali sana kitaaluma
kutokana na ufundishaji mzuri na mvuto atakaoendelea kuupata
katika sanaa hii ya mapigano.

No comments:

Post a Comment